August 3, 2017


                      
Uongozi wa Yanga umeonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutoalikwa katika hafla ya ukabidhi wa vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.

Wakati wa kukabidhiwa jezi hizo, leo. Yanga haikuwa na mwakilishi na badala yake, Msemaji wa Simba, Haji Manara akafanya “uchale”, kwenda kuwa sehemu ya mwakilishi wa Yanga wakati vijana husika wakionyesha jezi za Yanga za msimu ujao, jukwaani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia hilo amesema wamesikitishwa na jambo hilo na hasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania, wameonekana kutowatendea haki.

"Hicho kitendo kimetusikitisha sana, kiuweli hali hiyo inatufanya tuonekane wazembe kwa mashabiki wetu kutokana na TFF ambao ndiyo waratibu.

"Niseme kuwa, TFF haijatupa mwaliko wa aina yoyote ikiwemo email (barua pepe), simu na hata kutufuata hapa ofisini kwetu maana siyo mbali kutoka hapo ofisini kwao.

"Kiukweli kitendo kimetusikitisha sana na kingine ninashangaa hao TFF hizo jezi zetu wamezitoa wapi? Kwa sababu hizo zilipelekwa kwa mmoja tuliyempa tenda ya kuziwekea logo, hiyo inamaana waliptia mlango wa nyuma na kutuzunguka kuchukua jezi bila ya kututaarifu washusika.

"Kitendo hicho huenda wenyewe TFF wakakiona kidogo lakini kwetu ni kikubwa na huenda kikaleta mpasuko klabuni kwetu,” alisema Mkwasa akionekana kutofurahishwa na jambo hilo.


“Kingine hao TFF kwanini wanapotukata makato yetu wanatoa taarifa, lakini hili la kukabidhiwa jezi wameshindwa kututaarifu," aliendelea kusisitiza Mkwasa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic