October 26, 2017



Na Hussein Rashid, Unguja
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ameonekana akiwa fiti wakati timu hiyo ilipofanya mazoezi leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba ilifanya mazoezi katika uwanja huo huku mvua ikiendelea kunyesha.

Okwi alionekana kuwa fiti kutokana na kukimbia kwa kasi licha ya uwanja huo kuwa na maji yaliyotuama.

Simba inajiandaa dhidi ya watani zake Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.


Mechi hiyo ya watani itachezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic