October 26, 2017


Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesisitiza suala la utulivu na kufuata utaratibu kwa mashabiki watakaokwenda uwanjani.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, keshokutwa Jumamosi.

Mkwasa amesema mashabiki wanatakiwa kufuata utaratibu ili kuhakikisha mpira huo unaisha kwa amani.

“Wao wakifuata utaratibu basi mambo yataenda vizuri kabisa. Kila mtu afuate utaratibu,” alisema.

“Kama shabiki atakuwa hana tiketi basi ahakikishe haji uwanjani maana hatapata nafasi ya kuingia.

“Vizuri kila mmoja ajue suala la usalama linamhusu,” alisisitiza Mkwasa.

Jana, Mkwasa alisema Yanga ina nafasi za mashabiki 11,000, hivyo wanatakiwa kukata tiketi mapema.


Uwanja wa Uhuru unaingiza hadi watu 23,000 waliokaa vitini hali inayozua mzozo mkubwa kwa kuwa mashabiki wangetaka kwenda kwa wingi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic