March 26, 2018





Huku Simba ikiwa katika maandalizi yake ya mwisho kabla ya kuivaa Njombe Mji na baadaye Yanga, hofu imeibuka.

Hofu imeibuka kutokana na kiungo wake mkabaji, Jonas Mkude kuumia.

Mkude ameshindwa kumaliza mazoezi ya leo ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani baada ya kugongana na mwenzake, Muzamiru Yassin wakati wakiwania mpira.

“Ajali” hiyo ililazimisha Mkude kutolewa nje akiwa amebebwa na daktari wa Simba, Yassin Gembe akampatia matibabu.

Hata hivyo, haikujulikana aliumia kwa kiwango gani na kama ataweza kucheza mechi ijayo au na kwa kuwa daktari anaendelea na kazi yake na kesho, atajua usahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic