March 11, 2018

MMOJA WA VIONGOZI WA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE

Ukiangalia unaweza kuona Simba wako kimya lakini wanafuatilia kwa ukaribu nyendo za Al Masry.

Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuna watu ambao tayari wako mjini Port Said nchini Misri kuhakikisha Simba inapata kila kitu.

"Unajua mechi ya marudiano ni siku chache tu zimebaki, hivyo kila kitu cha maandalizi ya Al Masry, Simba wanataka kujua.

"Kinafuatiliwa na tunajua mchezaji yupi yupo, nani hayupo kuhusu vitu vyote na wanachotaka kufanya.

"Kuna mengine siwezi kukuambia ni nini lakini Simba wanafuatilia na kuna watu hapa. Mmoja ni kocha wa juu tu na anajua mambo yote ya mpia," kilieleza chanzo kutoka Cairo.

Simba wako katika maandalizi ya mwisho kujiandaa kwenda Cairo na baadaye Port Said ambako mechi hiyo itachezwa.

Uongozi wa Al Masry tayari umeomba kuongezewa mashabiki kwenye uwanja wake ambao una historia mbaya ya kukosa ulinzi wa kutosha baada ya baadhi ya mashabiki kufikia uwanjani hapo kutokana na vurugu, miaka kadhaa iliyopita.

1 COMMENTS:

  1. Simba mara nyingi huwa na mipangilio mizuri ya kudili na warabu. Almasry walinufaika zaidi walipokuja nchini kutokana na baadhi ya watanzania kuwapa siri zote za Simba wakati Simba wakiwa hawana ufahamu mzuri wa adui wao. Lakini kitendo cha Simba kucheza nao mechi ya kwanza wamepata nafasi ya kumfahami mpinzani wake ingawa inawezekana kabisa kuwa Almasry waliwaacha baadhi ya wachezaji ili kuja kuwachezesha katika mechi ya marudiano iwe kama saprize ya kuwamaliza simba ugenini. Mimi kama mdau wa soka ningewashauri Simba wamuandae Juko Murshidi hizi Game za kimataifa ndio game zake atawasidia sana kuimarisha backline yao kwani katika mechi ya beki ilionekana kukosa umakini labda lilikuwa tatizo la uzowefu . Na kwa wale wachezaji wengine wa Simba wanaotafuta njia za kusonga mbele zaidi katika maisha yao ya soka basi wakipata nafasi ya kucheza mechi kama hizi ndio za kufia uwanjani. Hakuna sehemu ya kujitangaza zaidi kama mchezaji wa soka Africa kwa sasa kama si nyumbani kwa akina Muhamedi Salah. Tuliwahi kusikia kichuya anatakiwa na Zamaleki sijui Alhal za Misri. Sasa nafasi imemjia bila ya kutarajia ya kwenda kuwathibitishia kuwa anaweza. Kichuya na Simba wakitusua mechi ya Almasry basi Zamaleki watakuwa hawana haja ya kumfanyia majaribio kichuya na thamani itapanda . Lakini ikitokezea kushindwa basi wasubiri mwakani kama simba watafanikiwa kuliwakilisha taifa tena Africa .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic