June 29, 2018




Unaweza kusema kuwa Kocha Hans van Der Pluijm ndiye ameshikilia mikataba ya wachezaji wa Waghana wa Azam FC, Daniel Amoah na Yahaya Yakubu baada ya kuwa majeruhi wa muda mrefu.

Amoah alipata majeraha ya goti na kutarajia kukaa nje kwa muda ya miezi tisa huku Yahaya Yakubu yeye alivunjika mfupa wa mguu, licha ya kuwa fiti kwa sasa lakini naye yupo kwenye hatihati ya kuachwa na timu hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema kuhusu masuala ya kuachwa kwa wachezaji na kuongeza mikataba yao, wanamsubiri kocha wao mpya ndiye atakayetoa maamuzi ya nani waendelee naye na yupi wamuache katika dirisha hili.

Source: Championi


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic