AJIBU AKOSA MAZOEZI SIKU NNE YANGA, ZAHERA AMVAA
Baada ya kuibuka na uhsindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC jana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema hakumpanga Ibrahim Ajibu kwa sababu alikosa mazoezi.
Zahera alieleza kuwa Ajibu katika siku 10 zilizopita alihudhuria mazoezi kwa siku nne pekee hivyo hakuona haja ya kumuweka kwenye kikosi dhidi ya Mwadui.
Kocha huyo ambaye alikuwa Congo kwa majuku ya timu ya taifa kama Msaidizi, amefunguka kwa kueleza kuwa hakuna mchezaji ambaye anaweza kuwa juu ya Yanga hata kama awe na jina kubwa.
"Unajua mimi siwezi kumpanga mchezaji ambaye anakuwa mzembe wa kuhudhuria mazoezi, Ajibu katika siku 10 amefika mazoezini mara nne pekee hivyo hakuwa na sababu ya kucheza" alisema Zahera.
Ajibu ameikosa mechi hiyo ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwa Yanga kucheza mechi nje ya jiji la Dar es Salaam kwa msimu huu kutokana na kushindwa kuhudhuria programu ya siku 4 za mazoezi.








0 COMMENTS:
Post a Comment