Uongozi wa Singida United, umesema kuwa tayari umekamilisha taratibu za kunasa saini ya mchezaji wa kimataifa mwenye uraia pacha wa Liberia na Norway Dauda Bortu.
Ofisa habari wa Singida United, Cales Katemana amesema wanafanya usajili kwa umakini kuweza kusuka kikosi kipana.
"Tumeingia mkataba na mchezaji wa kimataifa Dauda Bortu kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo wengine wanne wa kimataifa wapo njiani kuja," alisema.
Wachezaji ambao waliondoka katika kikosi cha Singida United ni pamoja na Jamal Mwambeleko na Peter Manyika ambao wapo nchini Kenya.








0 COMMENTS:
Post a Comment