December 17, 2018



Kocha wa Azam FC, Hans Pluijm amesema anajivunia uwezo wa wachezaji wake ndani ya kikosi anaamini watapata matokeo katika michezo yao ijayo kutokana na aina ya wachezaji alionao ikiwa ni pamoja na Chirwa.

Pluijm ambaye katika dirisha dogo amesajili wachezaji wawili ambao ni Obrey Chirwa aliyetoka Nogoom El Mostakbal ya Misri na Stephan Kingue akiwa ni mchezaji huru mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Kwa sasa hatuna haja ya kuwa na presha na matokeo tunayoyapata, kazi yetu kubwa ni kujenga timu ambayo itaweza kupata matokeo mazuri ambayo ni kipaumbele chetu kuelekea katika kuutafuta ubingwa wa ligi kuu," alisema.

Wachezaji wanne wametoka Azam na kujiunga na timu nyingine ambao ni Mbaraka Yusuph (Namungo FC) Waziri Junior (Biashara United), Ditram Nchimbi (Mwadui FC) na Abdul Omary (Mbao).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic