May 6, 2019


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hata kama akipita Yanga leo ama Lipuli watakachopokea kwao ni kichapo tu kwenye hatua ya fainali kwani kwa sasa wao hawana presha.
Akizungumza na Saleh Jembe, mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa kwenye michezo kuna matokeo ya aina nyingi hivyo wao hawana hofu na atakayepita leo kwenye mchezo kati ya Lipuli na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Samora.
"Tumepita na kutinga hatua ya fainali, kilichobaki ni kumsubiri mshindi kati ya Lipuli na Yanga, apite Lipuli kwetu sawa, apite Yanga kwetu sawa ila tutakayekutana naye kwenye fainali ni lazima tumchape na kombe tunabeba.
"Kazi ya kwanza  ambayo ilikuwa ngumu tulianza na kombe la Mapinduzi tumebeba, hapa kwenye ligi bado tuna mechi za kumalizia ni lazima tufanye vizuri, ila hili la Shirikisho hamna namna tumelikosa muda mrefu sana tutapambana kushinda," amesema Alando.
Azam FC hawana bahati na timu zote mbili kwani msimu huu walipocheza na Lipuli michezo miwili ya Ligi Kuu yote wametoka sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa kwanza kwa Yanga uliochezwa Uhuru walipoteza kwa kufungwa bao 1-0, hivyo itakuwa ni fainali ya kisasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic