May 6, 2019


Imeripotiwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema anataka kuongeza wachezaji wanne tu msimu ujao.

Aussems ameyasema hayo baada ya mchezo wa jana katika Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons kumalizika huku wakishinda kwa mabo 1-0.

Kocha huyo amesema ana malengo hayo ya kusajili ikiwa ni pamoja na beki wawili kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja kwa ajili ya michezo ya klabu bingwa Afrika.

Aidha kocha huyo amesema ligi kuu ya Tanzania haina ubora mkubwa kwa sababu timu nyingi ni dhaifu.

Aussems amedai kati ya timu 20 unaweza ukakuta timu 5 tu ambazo zina ubora wa kushindana sawa ila zingine ni dhaifu ndio maana wanashinda kwa urahisi hali inayowapelekea kupata changamoto kubwa wanapotoka nje ya nchi.

5 COMMENTS:

  1. Wanashindaje kiurahisi wakati marefa wanawabeba!? Viongozi wanatoa rushwa!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kuna timu inabebwa Tanzania kuliko zote ni ya Yanga!Leo wanacheza FA na Lipuli...unajua ilifikaje.Katika mechi yake na IHEFU zilionfezwa dak 15 na Yanga alipata goli la ushindi katika muda huo.Juzi na Azam , penalty na goli halali vimekataliwa!

      Delete
  2. Kinachowabeba Simba sio mapendeleo ni kutokana na ubora WA kikosi cha mabilioni, ubora WA Idara na si umeona jinsi Mnyama alivofika robo fainali na kuwalaza hata mabingwa WA Africa au ndio wamependelewa? Pia morali kubwa Sana ya wachezaji huku wakilipwa haki zao na malupulupu ya ajabu bila ya kucheleweshewa na kupelekea ugomaji. Yote hayo ni kiumbe gani mwenye akili timamu na asiyekuwa na hasadi au chuki anayethubutu kutamka hayo?

    ReplyDelete
  3. Naungana kabisa na kocha kwenye nyongeza ya wachezaji wanne wa ziada ambao sio wa kufanyiwa majaribio bali ni wakujulikana kabisa uwezo wao. Idadi alioitaja kocha kwakweli ni ya kitaalam zaidi kwani inaonesha wazi kuwa kocha hana nia ya kukibomoa kikosi cha sasa bali anania ya kutaka kukiimarisha zaidi, safi sana.

    ReplyDelete
  4. fikiria tunacheza na yanga badala ya kucheza mpira wanapaki basi tunahitaji timu ambazo zitatupa changamoto sio zinazocheza mpira kwenye vyombo vya habari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic