May 6, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa atatumia dakika 15 kumaliza mchezo wa leo dhidi ya Lipuli utakaochezwa uwanja wa Samora ikiwa ni hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa , wanaitambua Lipuli namna inavyopambana kutafuta matokeo hivyo ili kupata ushindi ni lazima wapambane kushinda mapema kabla ya kwenda mapumziko.
"Namna ambavyo Lipuli wanacheza pamoja na kikosi changu kilivyo ni lazima tupambane kupata matokeo mapema, nimewaambia wachezaji wangu ndani ya dakika 15 mpaka 20 wanatakiwa wafanye juhudi kutafuta matokeo kisha tukienda mapumziko tutakuwa na jambo lingine la kufanya.
"Kama mchezaji atashindwa kufuaa maelekezo ndani ya dakika hizo sitaona taabu kumtoa ila ninaamini tupambana kwani mchezo wetu wa mwisho wa ligi tulipoteza na niliwapongeza wachezaji kwani walipambana licha ya kupoteza," amesema Zahera.
Mshindi wa mchezo wa leo atatinga hatua ya fainali ambapo atacheza na Azam FC ambao wao walishinda mbele ya KMC ushindi wa bao 1-0.

1 COMMENTS:

  1. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic