May 6, 2019


MCHEZO wa Leo hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Lipuli FC ya Iringa na Yanga utakaochezwa uwanja wa Samora umebadilishwa muda kutoka saa 10:00 mpaka saa 9:30 Alasiri.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha mpira Iringa (IRFA), Ally Ngala amesema kuwa sababu kubwa za kubadili ratiba za mchezo huo ni kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe na kama itatokea sare baada ya dakika 90 kukamilika na muda wa ziada kabla ya kufikia hatua ya penalti.

"Kama itatokea sare kwenye mchezo wa leo ambao utakuwa na ushindani na endapo muda wa nyongeza utakamilika bila kumpata mshindi basi tutakwenda kwenye changamoto ya penalti," amesema.

Viingilio vya mchezo wa leo utakuwa  kama ifuatavyo :- V.I.P  20,000, mzunguko 5,000 na watoto watalipa 2,500 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic