May 6, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa dawa ya kuishusha Yanga kileleni ni kushinda mechi zao zote kama ambavyo wao walifanya kujikita kileleni.
Simba wamejikusanyia pointi 78 wakiwa nafasi ya pili huku mpinzani wao Yanga akiwa kileleni na pointi zake 80 wakitofautiana michezo ya kucheza ambapo Yanga imecheza michezo 34 na Simba imecheza michezo 30.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kagere amesema kuwa hakuna namna itakayowashusha Yanga kileleni zaidi ya wao kushinda mechi zao watakazocheza kwenye ligi.
"Unajua wenzetu wanaongoza kwa kuwa walishinda mechi zao na kupata matokeo, hivyo nasi hatuna kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kushinda ili kuwashusha pale walipo nasi tuongoze kama wao.
"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila mmoja anahitaji matokeo, tuna kazi kubwa na tunapambana kupata matokeo, kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuwa tunaendelea kupambana na mashabiki wasichoke kutupa sapoti," amesema Kagere.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic