May 20, 2019

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa amejipanga kubeba pointi tatu kesho uwanja wa Namfua watakapomenyana na Singida United.

Aussems amesema kuwa kwa sasa anahitaji pointi moja pekee ili atwae ubingwa hivyo ataugeuza mji wa Singida kuwa sehemu ya kifalme kwa mashabiki wa Simba.

"Kwa sasa nahitaji pointi moja ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo mchezo wetu dhidi ya Singida United ni muhimu kwetu kubeba ubingwa.

"Mashabiki wa Simba waliopo Singida ni muda wao kuwa wafalme, hivyo tutaugeuza mji wa Singida kuwa mji wa kutwalia ubingwa wetu," amesema Aussems.

Simba imetiia timu leo Singida United kwa ajili ya mchezo wao utakaochezwa kesho, wakiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa mabao 3-0 mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic