SINGIDA WAITISHA SIMBA
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amewaambia Simba kuwa uwanja wa Namfua siyo mahala pa kutangazia Ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.
Sanga amewaambia Simba watafuta sehemu nyingine na sio Namfua kwa kujiamini amedai kesho Simba watataga mayai matatu na kuacha pointi tatu Singida.
Kauli ya Sanga imekuja kufuatia timu hizo zitakuwa na mchezo wa ligi kesho kwenye uwanja huo majira ya saa 10 kamili jioni.
Kuelekea mechi hiyo, Simba wanahitaji alama mbili pekee kunyakuwa ubingwa wa ligi kwa mara ya pili mfululizo.
Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili salama mjini Singida na leo jioni kimefanya mazoezi tayari kwa mchezo
Wee piga kelele kesho utalia machozi ya mvua
ReplyDeleteametumwa na bosi wake
ReplyDelete