August 13, 2019



BAADA ya KMC kulazimisha suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Kigali ya Rwanda leo kinaanza mchakato wa kuwainda wapinzani wake.

AS Kigali ya Rwanda imemsajili nyota wa zamani wa Yanga na Simba Haruna Niyonzima ambaye alimalizana na Simba msimu uliopita.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa baada ya kikosi kurejea kocha alitoa mapumziko ya siku moja.

“Kikosi kilirejea salama Jumapili, na Kocha Mkuu Jackson Mayanja akawapa wachezaji siku moja ya kupumzika leo wanaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya AS Kigali.

“Kuna mengi ambayo tumejifunza na benchi la ufundi limeyaona na linayafanyia kazi, kwenye mchezo wetu wa marudiano hakuna namna lazima tushinde tu mashabiki watupe sapoti,” amesema.

KMC inatarajiwa kurudiana na AS Kigali kati ya Agosti 23-25 jijini Dar. 

1 COMMENTS:

  1. Tangazani viingilio rafiki ....mapema ili watu waje wengi uwanjani kuwasaport.As Kigali nitimu yakawaida sanaa...viingilio vikiwa rafiki then uwanja utajaa na mtapatasaport ...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic