August 13, 2019


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kikosi kinajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudio wa kimataifa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

 Mwakalebela amesema Yanga imeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utakaopigwa Agosti 23 nchini Botswana.

Mwakalebela amesema wakiwa kambini, watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (Agosti 16) na AFC Leopards (Agosti 18)


"Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amewasema kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers hivyo matumaini  ya kupata ushindi ni makubwa," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Mkuu kuna giza hapa ila pazia likifunguliwa watu watapigwa na butwaa kwanini waliwachagua hawa viongozi....Yanga amkeni muichunguze na kuwa karibu na timu yenu......maswali ni mengi kuliko majibu.....ukianzia na kwanini Mwl Zahera achelewe kujiunga na timu hali akijua CAF CL imetoka na timu ni mpya anatakiwa awepo ili aiandae....kwanini madai ya wachezaji wanaodai kutoka msimu uliopita viongozi hawajayafanyia kazi....suluhisho la haya kwanini hayapatikani.....timu inatakiwa iwe imeshatuma watu botswana je wameshafanya hili?

    ReplyDelete
  2. Kwanini Balama Mapinduzi hayupo kambini Moshi? Haya maswali na wasiwasi wa mashabiki yanazidi kuvuma yaani pale ambapo mchezaji fulani anaanza kuwa tegemeo hapo ndipo mambo yanaanza kuzuka, mara majeruhi mara ana matatizo binafsi/kifamilia....ili mradi figisu figisu....wana Yanga sio wajinga wanajua kila Kinachoendelea kuna siku watatoka mafichoni na kuleta sintofahamu

    ReplyDelete
  3. Yanga yanga yanga, viongozi mlio madarakani angalieni yawezekana kuna mbinu mbaya za kuiangusha club. Maadui wapingwe kabisa.

    ReplyDelete
  4. Hakuna mbinu yeyote .Ukosefu wa akili tu.Unapeleka timu Moshi kama kweli iko Moshi .Moshi ni joto kama Dar kwanini kambi isiwe Arusha?
    Kama suala ni hali ya hewa mbona hali ya hewa ya Gaberone ni karibu sawa na Dar kwa kipindi hichi hamna baridi la hivyo?
    Ingebaki Morogoro.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic