KIUNGO wa
kimataifa wa Zesco United ya Zambia, Anthony Akumu raia wa Kenya amefichua kuwa
wamejipanga vizuri kuisambaratisha safu ya kiungo ya Yanga inayoongozwa na Papy
Tshishimbi na Abdulaziz Makame kwa kuwa
ndiyo walikuwa kikwazo kwao.
Akumu ametoa
kauli wakiwa kwenye maandalizi yamwisho ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa
Afrika dhidi ya Yanga utakaopigwa leo nchini
Zambia baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa
Taifa, Dar.
Akumu amesema tayari wameshaanza wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika mchezo wa
marudiano kwa kuwa wameshatambua udhaifu wa wapinzani wao.
“Tunaendelea na maandalizi tunatambua kwamba wapinzani wetu Yanga walitubana zaidi
kwenye eneo la kati hivyo tunajipanga kufanya vema.
"Unajua katika kipindi cha kwanza wao walichofanya kwa eneo la kati ni kumtumia
yule mwenyewe namba 21 (Makame) ambaye alikuwa akitokea pembeni kuja kati
kuvuruga na hata yule nahodha wao (Tshishimbi) maana muda mwingi walifanya kati
kuwe kugumu lakini naamini kwa maandalizi yetu ni lazima tushinde,” amesema
Akumu.







Always we say the time will tell, lets wait.
ReplyDelete