December 28, 2019



JKT Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Abdalah ‘Bares’ imegoma kufanya usajili msimu huu wa usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16.

Kwa sasa JKT ipo nafasi ya saba ina pointi 19 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 13 ilishinda mechi tano na kupoteza mechi nne na kutoa sare nne.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa kwa sasa wanatambua dirisha limefunguliwa ila hawana presha ya kufanya usajili zaidi ya kuwatumia wachezaji wake wa kikosi cha vijana.

“Nina kikosi cha vijana ambao wana uwezo mkubwa ndani ya timu hvyo nitakachokifanya ni kuwapa nafasi wale ambao nitakuwa ninawahitaji kuhusu usajili kwa sasa sifikirii kuwa na ingizo jipya.

“Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anatambua kwamba ligi ya msimu huu ni tofauti na msimu uliopita kikubwa ni kutambua kwamba wachezaji wanamajukumu yao ndani ya uwanja na benchi la ufundi nalo linatimiza majukumu yake kwa wakati,” amesema Bares.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic