January 31, 2021


UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa haukuwa na mpango wa kuachana na Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba na alibwaga manyanga Januari 7.

Sven alisepa ndani ya Simba mazima ikiwa ni siku moja baada ya Januari 6 kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum umewapa tiketi Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Crestius Magori amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba,(Barbara Gonzalez) alipigiwa simu na watu kutoka sehemu aliyokuwa anakaa Sven na kuambiwa kuwa amebeba kila kitu mpaka viatu.

"Hatukuwa na mpango wa kuachana na Sven ila yeye mwenyewe aliamua kuondoka na CEO,(Barbara) alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mbona kocha amebeba kila kitu kutoka kwa watu wa sehemu aliyokuwa anakaa.

"Ilikuwa ni asubuhi wakati huo timu ilikuwa inajiaandaa kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi.

"CEO alimpigia simu Sven ambapo alisema kuwa bado yupo hana mpango wa kuondoka ila timu imeanza safari mchana ndipo anamwambia CEO kwamba kuna matatizo ya kifamilia anahitaji kuondoka.

"Hata ambapo aliambiwa kwamba kama ishu ni familia basi ilete hapa Tanzania kuna shule akasema kwamba ana ofa kibao ikiwa ni pamoja na Morocco ambapo ni karibu na Ublelgiji, sasa hapo hatukuwa na namna ikabidi tumuache aondoke," .

Sven kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco akiwa ni kocha mkuu na Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.

13 COMMENTS:

  1. kama amesha ondoka Sasa sisi tufanya je?

    ReplyDelete
  2. Hatukumngangania kwa kusema ana mkataba nasi wa miaka miwili hata kufikishana FIFA kama vile wanavofanya wengine na kaondoka kwa amani na kumtakia heri na huenda huyu tulienae ni bora zaidi na huu ndio uungwana

    ReplyDelete
  3. Hii bado ni stori ya kuandikwa? Hakuna habari mpya jamani? Ameshaondoka hilo limepita, maisha yaendelee. Yeye sio kocha wa kwanza simba na wala hakuwa special

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwandishi ni shabiki lialia wa utopolo na ndio maana kwake hii bado ni storh

      Delete
  4. Mikia aka Gubu...he he he

    ReplyDelete
  5. Unaesema mikia, wa kwenu aliondoka na kuwatukana juu, hatukusikia mkitapatapa, mmeyasikia ya wenzenu ndio kidomodomo, acha hizo kama wewe ni mtoto wa kiume!!

    ReplyDelete
  6. Eymael aliwaita manyani . Unategemea mazuri kutoka kwa manyani?Utopolo watupie ndizi. Je deni la Vincent mlilipa?Uhasidi ndio zao. Ngoma haiwahusu lakini ndio wakata viuno wakubwa.

    ReplyDelete
  7. Eti mikia au gubu, wakwenu aliondoka kwa shari na matusi juu na kusema hamnazo na akawaita majina ya yule mnyama anaebweka na yule mwizi wa mahindi shambani. Vyura bhana

    ReplyDelete
  8. Alikuwa kocha mzuri sana but anyway huyu pia atatufikisha mbali sana coz he has a skills in coaching a team so Simba we are going far

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic