MENEJA wa beki na nahodha wa
klabu ya Polisi Tanzania, Iddy Mobby aitwaye Joseph Assey amefunguka kuwa kiasi
cha Shilingi Milioni 50 ndiyo kinaweza kumng'oa mteja wake kutoka ndani ya
kikosi hicho.
Mobby amekuwa akitajwa kuhitajika na Yanga na Simba kwa ajili ya kujiunga nao ndani ya kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ili kuongeza nguvu katika vikosi hivyo.
Akizungumzia uhamisho wa nyota
huyo, Assey amesema beki huyo bado ana mkataba wa
miezi saba na Polisi Tanzania na inawezekana kuuvunja mkataba huo kama tu klabu
inayomuhitaji itatoa Shilingi Milioni 50.
"Mteja wangu Iddy Mobby bado
ana mkataba wa miezi saba na Polisi Tanzania, lakini hiyo haimaanishi kuwa
hawezi kusajiliwa na timu nyingine, kama kuna timu inahitaji huduma yake
basi italazimika kuvunja mkataba huo kwa kuleta dau la kuanzia Shilingi Milioni
50.
"Ni kweli Yanga wameonyesha nia ya
kumhitaji lakini siwezi kusema tumefikia katika hatua gani kuhusu dili
hilo,"
Mbona wakienda timu tofauti na Yanga au Simba hatuwaoni hao wanaojiita mameneja?
ReplyDeleteWa bei chee hao mchezaji wa kweli hapatikani kwa bei hiyo
ReplyDeleteKuna mchangiaji mmoja alitoa maoni yake ya kwamba kama itatokea blog nyingine ya habari za michezo basi hii blog itakufa kifo cha kimya kimya kwa habari zao za kuunga unga
ReplyDeleteSi uache kuifungua... kwani kuna mtu kalazimishwa hapa.. mikia aka paka mweusi
ReplyDeleteTunajua kuwa wewe ni mke wake SalehJembe na hapa unamtetea mumeo,katika hilo hatuwezi kukuzuia,tunachofanya sisi wasomaji wake ni kumpa nasaha na angalizo ili kuipa hadhi blog na kuifanya iaminike sasa wewe unaleta mipasho itakayochangia kumuangusha.Wenzetu wenye weledi huzingatia sana maoni na ushauri wa wateja na kuyafanyia kazi
Delete